WAWEKEZAJI wanaokuja kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini, wameandaliwa rasimu mikataba elekezi baada ya kubainika baadhi ya mikataba wanayokuja nayo, inaleta usumbufu.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
WAKATI serikali ikianza kutafuta suluhisho la kudumu la matatizo wafanyabiashara ndogo, mama lishe kuhusu upatikanaji wa maeneo, imebainika kuwapo mchezo ‘mchafu’ wa wafanyabiashara wakubwa kutumia mgongo wa wamachinga, kusambaza na kuuza bidhaa zao maeneo yasiyoruhusiwa.
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya kwa kutengua uteuzi wa wakuu wa wilaya 12, kuteua wapya 27 na wengine 64 kubadilishwa vituo vyao.
WATU wanne wamekufa na wengine wanne kujeruhiwa na kulazwa katika kituo cha afya cha Mtakatifu Joseph kilichopo kata ya Dumila wilayani Kilosa mkoani Morogoro, baada ya kuzuka kwa mapigano baina ya wakulima na wafugaji.
SERIKALI imesema inachukua hatua mbalimbali zitakazozuia uwezekano wa mifuko ya hifadhi ya jamii kufilisika, kutokana na mifuko hiyo kuidai serikali kiasi cha Sh trilioni 1.8.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imeshikwa kigugumizi kuhusu suala la kushusha nauli ya magari ya abiria kwa kutoa sababu za kisheria pamoja na ukokotoaji wa tozo.
BAADHI ya wakazi wa jijini Tanga wamepongeza hatua ya awali iliyofikiwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na JWTZ kwenye operesheni maalumu ya kusaka wahalifu pamoja na silaha waliokuwa wamejifisha katika mapango ya Majimoto yaliyopo eneo la Mzizima Amboni, nje kidogo ya mji.
TANZANIA bado inakabiliwa na tatizo la watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ambapo kwa takwimu za hivi karibuni watoto waliotambuliwa kuishi katika mazingira hayo ni 897,913, wanaume wakiwa asilimia 53 na wasichana asilimia 47.
WAKALA wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), umesema mwaka jana kumetokea matukio ya ajali za kemikali 11 zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya 14 na uharibifu wa tani zaidi ya 250 za kemikali.
WAKAZI wa kijiji cha Uchindile wilayani Ifakara mkoani Morogoro wamepata umeme unaozalishwa kwa kutumia kuni baada ya kuzinduliwa kwa mtambo wa 10kW uliotolewa na kampuni ya kimataifa ya Camco Clean Energy.