RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Tanzania ziko tayari kushirikiana na Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Kuwaenzi Waasisi wa Taifa kutokana na mchango wao mkubwa kwa Taifa hili.
zaidi ya miaka 5 iliyopita
MTOTO Yohana Bahati mwenye ulemavu wa ngozi (albino), aliyetekwa katika Kijiji cha Ilelema wilayani Chato katika Mkoa wa Geita, mwili wake umekutwa ukiwa umefukiwa huku umenyofolewa miguu na mikono.
MAMLAKA ya Maji safi na Maji taka Dar es Salaam (Dawasco) imekamata mifuniko ya majitaka katika kiwanda cha nondo cha Iron & Steel cha jijini Dar es Salaam ikiwa ni hatua mojawapo za kuzuia uhujumu wa miundombinu ya majisafi na wizi wa maji.
WAKALA wa Hifadhi ya Taifa wa Chakula (NFRA) Kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa, inadaiwa na halmashauri mkoani humo zaidi ya Sh bilioni 1.3 zikiwa ni fedha za ushuru kwa mahindi waliyoiuzia wakala huyo kwa msimu huu wa kilimo.
MELI nyingine kubwa yenye urefu wa mita 209, imetia nanga katika Bandari ya Mtwara.
WAKALA wa Ukaguzi wa Madini Tanzania umeutaka umma kujiepusha na utoroshaji , magendo na biashara haramu ya madini, kwani hatua kali zitaendelea kuchukulia kwa yeyote atakayebainika au kukamatwa akijihusisha na shughuli hizo.
IMEELEZWA kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi duniani, hivyo kuwa miongoni mwa nchi 20 zenye uchumi unaopaa’ kwa kasi ulimwenguni, na ya 10 katika kundi la nchi zenye mafanikio hayo katika Bara la Afrika.
WANAFUNZI wa shule za serikali za kata zinazobezwa kwa kuitwa yeboyebo wametakiwa kuendelea kufanya vizuri waitoe kimasomaso Serikali isikashifiwe kwa jitihada zake za kuendeleza shule hizo.
WAFANYABIASHARA wa mahindi nchini wametakiwa kuachana na uchuuzi na kusaidia wakulima kupata kipato zaidi kwa kuanzisha viwanda vya kutengeneza bidhaa zinazotokana na mahindi.
MKUU wa Mkoa wa Katavi , Dk Ibrahim Msengi amewataka makandarasi kufanyakazi kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha wanayolipwa katika miradi wanayoitekeleza.