WATU saba wakazi wa Kijiji cha Mabwegere, pamoja na vijiji vingine vya Tarafa ya Magole, wilaya ya Kilosa , mkoani Morogoro, wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya watu watatu na kuwajeruhi wengine wanne kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji wa jamii ya Kimasai.