KITENGO cha manunuzi cha Shirika la Umeme (Tanesco), kimetakiwa kufanya kazi kwa umakini kuhakikisha ukosefu wa nguzo, nyaya na mita haujitokezi. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Muhongo, amesema hayo juzi, alipokuwa akizungumzia kukerwa na kile alichosema kuwepo tatizo sugu la ukosefu wa vifaa hivyo na kusababisha shirika hilo kulalamikiwa na wateja.