KAMATI nane za Bunge zinatarajiwa kwenda nje ya nchi kwa ziara za kikazi na mafunzo, huku zingine nane zikiendelea na shughuli mbalimbali nchini ikiwamo kutembelea miradi. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Deogratius Egidio, alisema Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala iko Nairobi, Kenya na baadaye itakwenda Ghana kwa mafunzo.