SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limesema ujenzi wa daraja la Kigamboni, upo katika hali nzuri, ingawa kuna changamoto ya wananchi kumi ambao hawajahama, kupisha ujenzi huo. Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa shirika hilo, Eunice Chiume alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.