SERIKALI mkoani Mbeya, inakusudia kuzichukulia hatua za kisheria kampuni zote za ulinzi zitakazotoa ajira kwa vijana wasio na sifa, ikiwa ni pamoja na kupata mafunzo maalumu ya ulinzi.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
MKAZI wa kijiji cha Mkakatika, Bahi, Dodoma, Nzije Komite (65), mwenye wake 16 na watoto 52 wengi wao hawajui majina, amekabidhiwa ramani ya nyumba itakayomwezesha kupata makazi bora na familia yake.
MKUTANO wa pili wa Amani na Usalama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika Bujumbura, Burundi umebaini kwamba ufinyu wa demokrasia, rushwa, ukiukwaji wahaki za binadamu ni miongoni mwa hatari za kiusalama katika kanda hiyo.
MKAZI wa Kijiji cha Kapalala Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi , Mele Seni (60) ameuawa kikatili kwa kukatwa mapanga kichwani na mgongoni na watu wasiofahamika wakati akiwa nyumbani kwake akiota moto, sababu kubwa ikielezwa kuwa mzee huyo alikuwa anatuhumiwa kwa ushirikina.
MKANDARASI anayejenga barabara ya kiwango cha lami inayotoka Nzega hadi Puge mkoani Tabora amejikuta matatani baada ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza kukagua maendeleo ya mradi huo.
BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar imetakiwa kuongeza kasi ya ukusanyaji madeni kutoka kwa wahitimu waliokopeshwa na Bodi hiyo ili kuongeza uwezo wa Bodi kutoa mikopo zaidi kwa wanafunzi.
ALIYEKUWA mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, marehemu Dk Sengondo Mvungi ametajwa kuwa nguzo muhimu katika Tume hiyo kutokana na mchango wa ziada aliokuwa nao kulinganishwa na wajumbe wengine.
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu amesema maendeleo ya kweli ya jamii yatafikiwa endapo Serikali itashirikiana na Asasi za Kiraia katika kutatua changamoto za wananchi.
SIKU chache baada ya Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM) kutuhumiwa kumbaka msichana wa miaka 16, mwenyewe amekanusha kutenda jambo hilo na kudai kuna wanasiasa wenzake wanamchafua kisiasa.
MKUU wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Anthony Mtaka amewataka madiwani na viongozi wengine kuacha kuingiza masuala ya siasa kwenye mgogoro wa wafugaji na wakulima kwani hakutaleta suluhisho la kudumu.