RUFAA ya Janeth Manjuru (32), mke wa mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha, Jackson Manjuru anayedaiwa kutaka kumuua mumewe, jana ilikwama kusikilizwa. Ilikwama baada ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, M.P.Mwaimu kutaka mawakili wa awali wa mwanamke huyo, kwenda katika mahakama hiyo kueleza kama wamejitoa katika kesi hiyo kwa mdomo ama kwa maandishi.