MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wilaya ya Morogoro, Aziz Abood amesema baada ya mawaziri kubanwa na hata kujiuzulu au uteuzi wao kutenguliwa, sasa ni zamu ya kuondoa viongozi mizigo Morogoro.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
MKUU wa Mkoa wa Kagera, Fabian Massawe ameelezea kutishwa na kasi ya maambukizi ya Ukimwi mkoani mwake.
KAZI ya kulea watoto yatima katika Kituo cha Mgolole, iliyoanzishwa na Masista wa Moyo Safi wa Maria wa Morogoro mwaka 1937 wakiwa na mtoto mmoja, kwa sasa inakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo ya uhaba wa fedha za matibabu ya watoto hao yatima.
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limepiga marufuku ulipuaji wa fataki wakati wa sherehe za mkesha wa Mwaka Mpya, kutokana na sababu za kiusalama.
MRADI wa ujenzi wa bomba la gesi umetengeneza ajira mpya 400 kwa vijana tangu ulipoanza Agosti.
NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amesema Serikali haitavumilia baadhi ya askari Polisi wanaonyanyasa waendesha pikipiki za ‘bodaboda’.
ASILIMIA 96.15 ya wanafunzi wa darasa la saba waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu na kufaulu, ndio waliochaguliwa kujiunga na sekondari za serikali.
WAFANYABIASHARA na watumiaji wa Soko Kuu la Majengo katika Manispaa ya Dodoma, wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko baada ya miundombinu ya mifereji ya maji machafu kuziba.
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa amelitaka Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora kutumia Sh bilioni 2.3 za ushuru wa huduma kutoka katika mgodi wa dhahabu wa Resolute kwa miradi itakayosaidia maendeleo ya wananchi.
MBUNGE wa Jimbo la Tarime, Nyambari Nyangwine (CCM) amekanusha uvumi kuwa amehongwa ili asiwatetee baadhi ya wananchi wa jimbo hilo, ambao wako kwenye mgogoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA).