POLISI mkoani Morogoro inawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kusafirisha maiti akiwa na kete 17 tumboni kati ya 24 zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya wakitokea mjini Tunduma, mkoani Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
HALMASHAURI ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma inatarajia kuuza viwanja 3,000 kwa ajili ya makazi.
WATU wawili wamekufa maji jijini Dar es Salaam katika Sikukuu ya Krismasi akiwemo mtalii kutoka China aliyekufa wakati akiogelea na wenzake katika Hoteli ya Golden Tullip jijini Dar es Salaam.
WAUMINI wa madhehebu ya Kikristo katika Jimbo la Kanisa Katoliki la Tunduru/ Masasi, wamehimizwa kudumisha upendo, amani na utulivu ili kutoa nafasi ya maendeleo kutawala miongoni mwa jamii.
MFUMO wa usimamizi na utekelezaji wa shughuli za mawaziri nchini, umedaiwa kuhusika kuwaandalia mazingira ya kupoteza nyadhifa zao mara kwa mara.
WAKAZI wawili wa vijiji vya Nyabisaga Kata ya Pemba wilayani Tarime mkoani Mara, Mhoni Chacha Ng’wena (25) na Isack Magawi Meng’anyi (30), wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
WATU saba wamekufa katika mikoa ya Njombe na Pwani katika ajali za gari na mtoto kutumbukia kwenye ndoo.
NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Januari Makamba, ametaka viongozi wa dini kuwa makini na wasaka uongozi kwa kuwa Taifa linahitaji uponyaji kwa changamoto zinazolikabili.
BAADA ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri watatu na mmoja kujiuzulu, kutokana na kashfa zilizotokana na Operesheni Tokomeza Ujangili, viongozi hao wamezungumza yaliyowasibu kila mmoja kwa staili yake.
ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma Mhashamu Gervas Nyaisonga amewataka wananchi kutii sheria zilizowekwa na mamlaka ya nchi.