BAADA ya kushindwa kwa upotoshaji uliofanywa na wajumbe wa kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), linaloongozwa na Chadema na CUF na hoja zao kuanza kupoteza mwelekeo, wajumbe hao wameamua kufungasha virago kurejea makwao kujipanga kutafuta huruma ya wananchi. Wajumbe hao wamefikia uamuzi huo jana, baada ya kukaa Dodoma na kuchukua posho za siku zote za awamu ya kwanza ya Bunge Maalumu mpaka Aprili 30 mwaka huu, walizozitumia pamoja na mambo mengine kukashifu waasisi wa Muungano uliodumu kwa miaka 50 sasa, Mwalimu Julius Nyerere na Shekhe Abeid Amaan Karume.