BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekusanya zaidi ya Sh bilioni 49.7 ya mikopo kutoka kwa wanufaika wa mikopo hiyo hadi kufikia Aprili 30, mwaka huu.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema tuhuma za rushwa zinazoambatanishwa na kazi ya usaili wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji ni hisia tu za wahusika.
IMANI potofu ya kuunganishwa na dini inayodaiwa kuabudu shetani (Freemason) nusura ivuruge kazi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) ya kuandikisha majina ya kaya masikini, Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida.
BAADHI ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wamelaani kitendo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara, Venance Mwamengo cha kukanyanga kwa gari bidhaa walizokuwa wakiuza nje ya Soko Kuu la Tarime.
MMEA wa asili unaostawi kwa wingi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kitulo, maarufu kwa jina la Chikanda, upo hatarini kutoweka kutokana na kuvunwa kiharamu na watu wanaoamini unasaidia kupunguza makali ya Ukimwi.
WAZIRI wa Nchi asiye na Wizara Maalum Profesa Mark Mwandosya amewapoza watu wanaoshindwa katika uchaguzi kutokana na wapinzani wao kutoa rushwa kwa kuwaambia wanapaswa kuwa na amani, ipo siku wataonekana kutokana na usafi wao.
SAFU mpya ya uongozi wa Taifa ya Chama cha Wananchi (CUF) inatarajiwa kupatikana mwezi huu katika uchaguzi utakaofanyika wiki ijayo, jijini Dar es Salaam.
SHIRIKA la Usafiri Dar es Salaam (UDA) limekubaliana na Mamlaka ya Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra) kuweka vibao katika mabasi yake kuonesha njia yanakotoa huduma na si kupaka rangi. Mkuu wa UDA, Hamdy Al Hadj alisema kibao kitakachowekwa kitakuwa na rangi ya eneo husika kama ilivyo kwa daladala nyingine.
RAIS Jakaya Kikwete amelitaka Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwafikisha mbele ya vyombo vya haki watu wote waliohusika katika ulipuaji bomu lililosababisha kifo na kujeruhi watu saba mjini Unguja, Zanzibar.
WATUMIAJI wa kilevi cha shisha wako katika hatari kubwa ya kuugua maradhi ikiwemo saratani na kuathirika katika mfumo wa hewa . Wataalamu wa afya wameonya kwamba ulevi huo ambao kwa sasa umeshika kasi na kuteka watu wengi hasa vijana, una hatari kubwa kuliko uvutaji wa sigara.