KESI ya kikatiba iliyofunguliwa kutaka Mahakama iruhusu mbunge aliyefukuzwa uanachama katika chama chake atambuliwe kuwa Mbunge huru au aruhusiwe kuhama na ubunge wake kwenda chama chochote, imepangiwa jopo la majaji watatu.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
MAKAHABA takribani milioni moja wanaoishi Brazil wanatarajiwa kupata mapato makubwa wakati wa Kombe la Dunia lililoanza Alhamisi nchini humo.
WATU watatu wa familia moja ya Mzee Nyamachoma Gutu wa Kijiji cha Magoma Kata ya Binagi Tarafa ya Inchage, wamejeruhiwa kwa kukatwa mapanga na nyumba kuchomwa moto na kundi la watu waliodai kuwa ni wanandugu waliokuwa wakikusanya michango ya ndugu ya kusaidia familia ya koo hiyo.
VIONGOZI wa Serikali ya Mkoa wa Morogoro wametakiwa kuhakikisha Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHIF) inakuwa ni ajenda muhimu katika vikao vyao vya kitaalamu.
WANAKIKUNDI cha ufugaji nyuki katika kijiji cha Welamasonge wilayani Kwimba, mkoani hapa wamesema mnyama nyegere amekuwa changamoto kwao kwa kunywa asali kabla ya wao kurina.
WANAUME wametakiwa kufuata uzazi wa mpango kwa ajili ya kuimarisha familia zao na kupambana na hali ngumu ya maisha.
WANAUME wamehimizwa kuwasindikiza wenza wao ambao ni wajawazito kliniki wakati wa kupima afya zao na kuwa nao karibu wakati wote wa malezi ya watoto wao.
WATU wanne wamekufa mkoani Singida katika matukio mawili tofauti, likiwemo la wanandoa, vikongwe kuuawa kisha nyumba yao kuchomwa moto na mtu asiyefahamika.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeanza mchakato wa kuzipitia sheria zote zinazoonekana kupitwa na wakati ambazo zimekuwa zikiwadhalilisha wanawake na watoto.
WASOMI, wanaharakati na wananchi kwa ujumla wamepongeza Bajeti ya mwaka 2014/15 ya Sh trilioni 19 iliyowasilishwa bungeni juzi na kujikita zaidi katika kuimarisha miundombinu ya elimu, usafiri wa reli na usambazaji wa nishati ya umeme vijijini, wakisema imekata kiu ya Watanzania wengi.