WANANCHI wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Usafiri wa Nchikavu na Majini (Sumatra) kuondoa tatizo la magari ya abiria kupandisha nauli kiholela.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Issaya Mngulu na timu yake wamewasili mkoani hapa kwa ajili ya kufanya uchunguzi ili kubaini wizi katika vyama vya msingi vya ushirika ambapo zaidi ya Sh bilioni 12 hazijulikani zilipo mkoani Tabora.
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Anna Tibaijuka juzi alinusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kutoka Bukoba kwenda Dodoma kupata ajali kwa kugonga punda katika Kijiji cha Wendele wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni katika Mkoa wa Dar es Salaam imetenga Sh bilioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa masoko.
UONGOZI wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umesitisha safari za treni ya abiria kutokana na kutetereka kwa mojawapo ya madaraja katika Bonde la Mto Ruvu katika reli ya kati.
POLISI mkoani Mbeya inashikilia watu tisa wanaosadikiwa kuwa wapiga debe wakituhumiwa kufanya vurugu wakati mgomo wa daladala ulipokuwa ukiendelea jijini hapa.
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mbinga, Desderius Haule amekihama chama hicho na kujiunga na CCM.
KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Felix Maagi leo amekabidhi nyumba 40 ambazo zimenunuliwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) huku akizitaka taasisi nyingine kujitokeza kujengewa nyumba na shirika hilo.
POLISI mkoani hapa wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya machinga waliocharuka baada ya kuona vibanda vyao walivyojenga maeneo yasiyoruhusiwa vikibomolewa.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa, Sophia Simba amewataka Wenyeviti na Makatibu wa UWT wa Mikoa na Wilaya kutowalazimisha wanawake kutoa Sh 1,500 kwa ajili ya kununua kadi za uanachama.