WANANCHI katika eneo la Kivule, katika Wilaya ya Ilala wamesikitishwa na kauli ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kwamba madaraja yote katika Jiji la Dar es Salaam, sasa yanapitika, wakati eneo la Kivule bado halipitiki, baada ya kuharibiwa na mvua wiki iliyopita.