MAKATIBU Tawala wa Wilaya nchini wametakiwa kuwasaidia wakuu wa wilaya kuhakikisha chaguzi zote zinazokuja zinafanyika katika mazingira ya amani na utulivu kama ilivyo kawaida kwa Taifa.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
MKAZI wa Igoma, Mwanza, Leticia Moses (36) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya wizi wa Sh milioni 19.6.
MWANDISHI wa habari wa gazeti la Maua, Ibrahimu Kadino amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela au kulipa faini ya Sh milioni moja baada ya kupatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa.
ZAIDI ya wajasiriamali 200 wamejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Ziwa baada ya kupatiwa elimu juu ya manufaa na faida watakazopata baada ya kuwa wanachama.
WALIMU na wanafunzi wa shule za sekondari za Ibiri na Ilolangulu zilizopo mkoani Tabora, wamesema wamefurahishwa kuwezeshwa kupata mafunzo kupitia njia ya mtandao, kufuatia ushirikiano wa Airtel Tanzania na Mradi wa Millennium Village.
MUUZA mifuko, Malagira Jeremia (18) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, Dar es Salaam kujibu mashitaka ya kuingia kwa jinai ndani ya nyumba ya Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela jijini humo.
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema iko kwenye majadiliano na wadau wa vituo vya mafuta ya magari nchini, ili kuangalia namna bora ya kufunga mashine za kielektroniki za utoaji risiti kwenye pampu za vituo hivyo.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mjini Lindi mkoani humo, wamedaiwa kuweka mamluki wao katika Chama cha Wananchi (CUF) ili washinde kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa, zitakazoanza Oktoba mwaka huu na madiwani na wabunge mwakani.
SERIKALI imepiga marufuku utozwaji wa ushuru wa asilimia tano wa fedha za zao la pamba kutoka kwa wanunuzi kwa halmashauri 21 hapa nchini na badala yake, Serikali ndio itawajibika kulipa asilimia hiyo.
WATUMISHI 13 wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam, wametimuliwa kazi na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kwa tuhuma za kuchafua sura ya nchi mbele ya Jumuiya ya Kimataifa, kuendekeza rushwa na kunyanyasa raia wa kigeni.