TAFRANI iliyojitokeza bungeni juzi kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema kumuita Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila(NCCR Mageuzi) tumbili, naye kumjibu kwa kumuita mwizi imeingia katika hatua nyingine ambapo wawili hao wamekataa kusuluhishwa. Jana asubuhi baada ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, kuahirisha shughuli za Bunge, Mwenyekiti wa Bunge, Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan ‘Zungu’, aliwakuta Werema na Kafulila wakiendeleza mzozo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.