“NAMPENDA sana mke wangu, Prosista Laswai. Huyu ndiye injini ya mafanikio yangu, kitaaluma, kiutumishi, kisiasa na kimaisha kwa ujumla”, ni kauli ya Profesa Kitila Mkumbo (43), Profesa Mshiriki wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, katika Shule Kuu ya Elimu (DUCE).