HIVI karibuni, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, alikaririwa na gazeti moja akipendekeza kwamba ni vyema kukawa na vipindi vya kuachiana urais, kwa maana ya kwamba, endapo rais katika awamu fulani akitokea Tanzania Bara, basi awamu ijayo atoke Zanzibar.