UGONJWA wa ebola ni ugonjwa kama magonjwa mengine, ingawa watu wengi wamekuwa wakiuzungumzia kwa namna inayoonesha kuwa athari zake ni mbaya zaidi. Watu wanauzungumza wakionesha kwamba mwisho kwa mtu anayeambukizwa virusi vinavyousababisha, yaani kifo, kama vile ni tofauti na inayoweza kusababishwa na maradhi mengine, kama malaria, Ukimwi, kipindupindu na safura.