RASILIMALI watu katika taifa lolote duniani, ni moja ya nguzo kuu muhimu ya kuinua uchumi wa nchi husika, endapo wananchi wake watakuwa wamejengewa mfumo mzuri wa kurithisha maadili mema kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Kuna watu wanaoamini kwamba, kama unataka kuanzisha mgodi fulani, kwa mfano, unaweza kukodi teknolojia, lakini bado utahitaji nguvu kazi kama rasilimali muhimu sana ili uzalishaji ufanyike.