MOTO ni moja ya majanga yanayozikumba nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania na kusababisha majeraha na vifo, sambamba na kuathiri ustawi wa jamii kiuchumi na kimaendeleo. Madhara ya moto kila yanapotokea, yanatajwa kuwa chanzo cha umasikini na hata kuporomoka kwa uchumi kutokana na mazingira ambayo moto huo hutokea.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
MIAKA 38 iliyopita mfumo wa Ikolojia wa Selous-Mikumi ambao ni moja ya eneo lenye tembo wengi nchini ulikuwa na tembo 109,419 lakini tatizo la ujangili lililoikumba nchi limefanya idadi hiyo kupungua na kubaki tembo 13,084 tu kwa sasa. Hali hii ni hatari kwani kadri miaka inavyosonga ndivyo tembo wanavyouawa.
JUA la Kalahari halina huruma: Wasichana wawili na watoto wawili wenye umri wa kama mwaka mmoja hivi wako pekee yao chini ya mti wakijikinga na jua hilo. Ni katika eneo la New Xade, kambi ya wakimbizi ilio umbali wa saa moja kutoka mji wa karibu zaidi wa Ghanzi, Magharibi mwa Botswana.
SINABUDI kuanza makala haya kwa kuzishukuru nchi zilizoendelea ambazo kila kukicha huvumbua vitu vipya ambavyo havikuwahi kuwepo hapo kabla. Lengo la uvumbuzi mara zote limekuwa ni kumsaidia binadamu kuzidi kuyamudu vyema maisha yake.
CHUO Kikuu ni ngazi ya juu kielimu inayotegemewa na jamii mbalimbali duniani katika kutoa wataalamu. Kwa mantiki hiyo, jamii, serikali, wazazi pamoja na wanafunzi wenyewe katika ngazi hii huwa na matumaini makubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii mara watakapohitimu masomo yao.
DUMA ni mnyama wa familia ya felidae, yuko katika kundi la wanyama wanne wa jenesi Panthera maarufu kwa jina la paka wakubwa. Kundi hilo linajumuisha simba, chui na jaguar. Duma ambaye kitaalamu anafahamika kama Acinonyx jubatus anasifika kwa kuwa mnyama mwindaji mwenye mbio za kasi kuliko wanyama wengine wenye miguu minne.
MATOKEO mabaya ya mitihani ya mwisho ya kuhitimu elimu ya msingi ama ya sekondari katika Mkoa wa Rukwa ambayo yameendelea kuung'ang'ania mkoa huu kila mwaka yanaweza kuendelea endapo hatua stahili zitalegalega kuchukuliwa.
KWA kujua umuhimu wa kilimo katika nchi yetu ambayo bado uchumi wake hautegemei viwanda, kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikija na kaulimbiu mbalimbali pamoja na sera, lengo ikiwa ni kuhimiza na kuimarisha kilimo kwa maendeleo ya nchi yetu.
NYUKI, wadudu wanaotengeneza asali inayoaminika kuwa chakula chenye virutubisho vingi, wakifugwa kisasa wana nafasi ya kumwongezea mfugaji kipato chake pasi na shaka yoyote. Mbali na hilo, wanapofugwa kisasa wana faida nyingine kubwa ya kuhifadhi mazingira.
ILE dhana kwamba wawekezaji wengi katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga hawana faida kwa wananchi kwa kuwa hawashiriki ipasavyo katika kusaidia maendeleo, sasa inaonekana kutoweka baada ya migodi kuanza kutengeneza barabara za mji huu kwa kiwango cha lami.