“BABA Mandela amefariki na amepumzika kwa amani, taifa letu limempoteza mtu muhimu na wa pekee”, ni kauli ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini aliyoitoa Alhamisi usiku ,wakati akitangaza msiba wa Kiongozi shupavu na mwana wa Afrika wa kweli, Nelson Mandela (95), aliyefariki dunia usiku huo.