KWA mujibu wa takwimu, hivi sasa duniani watu milioni 15.9 kutoka nchi 151, wanajidunga dawa za kulevya aina mbalimbali kama vile kokaine, heroine, amphetamines na nyingine kama hizo, ambazo ni hatari kwa afya zao.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
WATU wengi hawahamisiki kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa kuwa wale waliokwishajiunga hukosa dawa mara kwa mara pale wanapougua, imefahamika. Wananchi hasa waishio vijijini wanaona hiyo ni kero kwao licha ya mara kwa mara kupewa matumaini ya kumalizika kwa tatizo hilo, hali inayofanya kuwa na mtazamo hasi juu ya kujiunga na mfuko huo.
HIVI Karibuni ilifanyika harakati za kuhamasisha Watanzania katika kujua namna nzuri ya kutumia na kuendeleza maisha yao kupitia mianya ya kimaendeleo inayowazunguka.
BANDARI ni nyenzo muhimu katika harakati za ukuaji wa kiuchumi kwa nchi yeyote iliyobahatika kuwa na rasilimali ya bahari.
MIRADI mingi inayohusisha kilimo cha umwagiliaji katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa ujumla imegharimu fedha zisizopungua Shmilioni 300.
WILAYA ya Mwanga mkoani Kilimanjaro inateketezwa na ukame wa muda mrefu ambao katika kipindi cha miaka 10 iliyopita dawa yake imekosekana kabisa.
MKUTANO wa 14 wa Bunge unaanza mjini Dodoma wiki hii huku Mkutano wa 13 uliopita ulimalizika kwa Bunge kupitisha Azimio la kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kutoa msimamo wa Serikali kuhusu kile kinachoonekana wazi kutengwa kwa Tanzania katika masuala kadhaa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
HAKUNA aliyeamini kwamba safari hiyo itafanyika. Uvumi uliokuwa ukiibuka miongoni mwetu, ni kwamba safari ndani ya maji imeahirishwa badala yake, tutasafiri kwa magari kutoka Mbambabay, Nyasa hadi Kyela.
RAIS Jakaya Kikwete alipohutubia Bunge tarehe 7 Novemba alisema kilichomleta bungeni ni suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na mustakabali wa Tanzania katika Jumuiya hiyo. Aliona umuhimu wa jambo hilo baada ya malumbano yaliyokuwa yakiendelea miongoni mwa wanasiasa na wananchi, pamoja na vyombo vya habari vilivyocharuka kuzungumzia kutengwa kwa Tanzania na nchi tatu jirani.
MUASISI wa kundi la waasi wa Lord's Resistance Army (LRA), nchini Uganda, Joseph Kony amezua gumzo katika ulingo wa siasa kutokana na taarifa zilizotolewa hivi karibuni kuwa anataka kujisalimisha.