MAPEMA mwezi uliopita Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ilitoa matokeo ya utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi Tanzania Bara, kwa mwaka 2011/12, ambapo yanaonesha hali ya umaskini kwa wananchi wa vijijini bado ni mbaya. Utafiti huo nchini hufanywa kila baada ya miaka mitano, na kwamba utafiti uliotangulia ulifanywa mwaka 2007, na kwamba katika utafiti huu wa sasa, maeneo tofauti 400 yakiwa ya mjini na vijijini yalifanyiwa utafiti.