MBALI na samaki, misitu, wanyama na gesi, rasilimali nyingine ya ardhini ambayo Mwenyezi Mungu kwa mapenzi yake aliamua kuwabarikia Watanzania ni madini ya aina mbalimbali. Vito na madini mbalimbali yanavyopatikana nchini mwetu ni mengi lakini kwa uchache ni pamoja na dhahabu, almasi, shaba, tanzanite na ruby.