CHUPA 450,000 za damu zinahitajika kila mwaka nchini ambapo kiasi kikubwa cha damu hiyo kinatumika kuokoa maisha ya mama na watoto. Hata hivyo chupa 150,000 tu za damu ndio zinapatikana na kusambazwa hivyo kuwa na upungufu wa chupa 300,000 za damu, hali inayosababisha uhaba mkubwa wa damu na akina mama na watoto kupoteza maisha.