LICHA ya Yanga kutolewa mapema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini mshambuliaji wake Mrisho Ngassa ndiye anayeongoza kwa upachikaji mabao mpaka sasa.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
FAINALI za shindano la kumpata mwigizaji bora mwenye kipaji (TMT) linatarajiwa kufanyika Jumamosi ya wiki hii kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Mratibu wa michuano ya Muungano, Daudi Yassin kusitisha uamuzi wake wa kustaafu kuandaa michuano hiyo.
IKICHEZA kwa kujiamini timu ya netiboli ya Shule ya Makongo jana ilitoa kipigo cha mbwa mwizi kwa timu dhaifu ya LCC Islamic ya Rwanda baada ya kuikandamiza kwa bao 107-4 katika Michezo ya tatu ya Shule za Sekondari ya Afrika Mashariki inayoendelea jijini Dar es Salaam.
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahmood Mgimwa anatarajiwa kuzindua rasmi shindano la Mwanamitindo wa Utalii Tanzania kwa mwaka 2014 Septemba 5 jijini Arusha.
TIMU ya netiboli ya Jitegemee jana ilizidi kudidimia shimoni katika Michezo ya 13 ya Shule za Sekondari za Afrika Mashariki inayoendelea jijini Dar es Salaam baada ya kupokea kisago cha mabao 63-11 kutoka kwa St Mary’s Kitende ya Uganda.
AKINADADA wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wametetea vyema ubingwa wao wa michuano ya Michezo ya Majeshi ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mchezo wa Netiboli ambao wanaushikilia kwa mara ya nane mfululizo sasa.
WASANII nchini wamekutana na uongozi wa Bunge Maalumu la Katiba kuwasilisha maombi yao mawili likiwemo la wasanii kutambuliwa kama kundi maalumu kama walivyotambuliwa makundi ya wakulima , wafugaji, na wavuvi.
WAKATI Yanga ikidaiwa kuandika barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumshitaki mshambuliaji wake Mganda Emmanuel Okwi kutokana na kukiuka masharti ya mkataba, Simba imesema haina nafasi ya mchezaji huyo kwenye kikosi chake.
MABINGWA wa soka Tanzania Azam wanaanza mazoezi rasmi leo kujiandaa na Ligi Kuu Bara pamoja na michuano ya kimataifa.