WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara amesema ili soka iendelee kuna haja ya kujifunza kutoka katika nchi zilizoendelea kwa kuwekeza kwa wachezaji wakongwe kwa manufaa ya baadaye.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
WASANII kutoka vyama vitano vya wasanii wamewasilisha mapendekezo yao yaingizwe kwenye rasimu ya Katiba mpya ambayo ni Haki miliki bunifu na kutambuliwa kama kundi kubwa la pili baada ya wakulima.
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) za mwaka 2017 baada ya Libya kujitoa.
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi mpya wa Mashindano kuanzia Septemba mosi, mwaka huu.
TIMU ya netiboli ya Jitegemee ya Tanzania jana ilianza vibaya Michezo ya 13 ya Shule za Sekondari za Afrika Mashariki (Feasssa) baada ya kupokea kichapo cha bao 29-23 kutoka kwa Shimba ya Kenya katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
WANAMUZIKI mbalimbali wameungana kutengeneza wimbo wa Siku ya Msanii ambayo itaadhimishwa Oktoba 25 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
TIMU ya soka ya Tanzania juzi ilinyang’ánya tonge kinywani timu ya Kenya kwa kuwalazimisha sare ya bao 1-1 katika michuano ya Michezo ya Majeshi na Utamaduni ya nchi za Afrika Mashariki inayoendelea visiwani hapa.
WACHEZAJI wakongwe wa timu ya Real Madrid ya Hispania juzi waliandika historia mpya katika Mkoa wa Kilimanjaro kutokana na kujionea maajabu ya mlima Kilimanjaro ukiwa na theluji yake isiyopungua pamoja na kutembelea maporomoko ya maji.
UJIO wa timu ya wachezaji wakongwe wa klabu ya Real Madrid unatarajia kuleta neema kwa Tanzania baada ya Serikali kusema kuwa imeanza mipango inayohusisha mazungumzo na klabu hiyo kwa ajili ya kuanzisha kituo cha michezo (Academy) kitakachobeba jina la timu hiyo hapa nchini.
LICHA ya Yanga kutolewa mapema kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini mshambuliaji wake Mrisho Ngassa ndiye anayeongoza kwa upachikaji mabao mpaka sasa.