UJIO wa Kombe la FIFA la Dunia nchini umesogeza mbele kwa muda usiojulikana Mkutano Mkuu maalumu wa marekebisho ya Katiba wa Riadha Tanzania (RT) uliopangwa kufanyika Jumamosi mjini Morogoro.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimesema kuwa dirisha dogo la usajili linatarajiwa kuanza rasmi Desemba 15, mwaka huu. Kazi hiyo ya mwezi mmoja inatarajiwa kukamilika Januari 15, mwakani.
KLABU ya soka ya Miembeni imesema kuwa inawanyemelea nyota wanne ambao watawasjili katika msimu wa dirisha dogo la usajili utakapowadia.
SERIKALI mkoani Kilimanjaro imeahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wadhamini na waandaaji wa mbio za nyika za Kilimanjaro Marathon, kutokana na umuhimu wake katika kukuza vipaji na uchumi wa mkoa.
KOCHA Msaidizi wa Kagera Sugar, Mrage Kabange amesema anasaka nyota wawili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi na kiungo katika kikosi chake.
KOCHA Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema anamsubiri Mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Rage arudi safari yake ya Ulaya, kisha azungumzie uamuzi wake wa kurudi kukinoa kikosi hicho cha Msimbazi.
TIMU ya soka ya Taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’ jana ilianza vema michuano ya Kombe la Chalenji baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Sudan Kusini.
TIMU ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ imeondoka nchini jana kwenda Nairobi Kenya katika michuano ya Chalenji inayoanza leo nchini humo.
KIUNGO wa timu ya soka ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars,’ Frank Domayo amesema ushindani umekuwa ni mkubwa katika kupata nafasi kwenye kikosi cha Taifa, kwani vijana wengi wamekuwa wakijituma na kuwaangusha wakongwe.
KAMPUNI ya Busara Promotions imeandaa onesho maalumu jijini Dar es Salaam kuonesha shoo za baadhi ya wasanii watakaoshiriki Tamasha la 11 la Sauti za Busara.