MWIMBAJI Solly Mahlangu wa Afrika Kusini amekubali kutumbuiza kwenye Tamasha la Krismasi linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya Dar es Salaam.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
KAMPUNI ya burudani ya Chief Promoters kwa kushirikiana na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wameandaa mafunzo ya siku moja kwa wasanii wa muziki, watayarishaji na wasambazaji itakayofanyika leo Dar es Salaam.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imezialika mabingwa wa soka wa Vietnam na Jamhuri ya Watu wa China kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Mapinduzi yatakayopamba maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofikia kilele Januari 12, mwakani.
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limezikumbusha klabu zote kuheshimu kanuni na kuzingatia muda wa usajili wa dirisha dogo la usajili ambalo linafungwa Desemba 15, mwaka huu, huku kukiwa hakuna klabu yoyoye hadi sasa iliyosajili mchezaji wa kigeni.
KOMBE la soka la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, linaanza leo nchini Kenya kwa wenyeji Kenya kuwakabili Ethiopia, ikitanguliwa na mechi ya Zanzibar dhidi ya Sudan Kusini.
MKURUGENZI wa Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo amehimiza wapenzi wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupiga picha na Kombe la Dunia la Fifa linalotarajiwa kutua nchini Ijumaa.
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema kuchaguliwa kwake kwenye Kamati ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), huenda kukajibu malengo yake ya kukuza soka la vijana Tanzania wakati ujao.
TIMU ya soka ya Benki ya Biashara ya Kenya (KCB Tanzania Ltd), imewatambia wenyeji wao, Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kuwafunga mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika mjini Unguja.
KUNDI la Muziki wa Injili la New Life Band la Arusha limethibitisha kushiriki Tamasha la Krismasi linalotarajia kuanza Desemba 25, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na mikoa mingine minne nchini.
KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imeeleza kufurahishwa na mashabiki wa burudani nchini kwa ushirikiano waliouonesha katika kufanikisha ziara na onesho la kundi maarufu la muziki la P Square kutoka Nigeria.