MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage amepewa siku 14 kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura ili kumaliza mgogoro uliopo ndani ya klabu hiyo kongwe nchini. Rais wa TFF, Jamal Malinzi aliwaambia waandishi wa habari jana, kuwa shirikisho hilo limefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuna mgogoro Simba kwani wamepokea barua mbili moja kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti huyo ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.