KOCHA Msaidizi wa Kagera Sugar, Mrage Kabange ameipa nafasi ya kunyakua ubingwa wa michuano ya Kombe la Chalenji timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars).
zaidi ya miaka 7 iliyopita
WASANII mbalimbali wa muziki wa Injili kutoka nchini wameomba kushiriki kwenye Tamasha la Krismasi litakalofanyika mwaka huu.
WANAFUNZI wa shule za msingi Mvumi Misheni na Chalula Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, wameiomba Serikali kurudisha vipindi vya ngoma za asili shuleni ili kudumisha utamaduni wa Mtanzania.
MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi ya Wizara za SMZ kwa mchezo wa netiboli yameanza juzi kwa mwenyeji wa mashindano hayo, timu ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais kuanza kwa kichapo.
MASHINDANO ya 19 ya Vijana ya Kombe la Muungano mwakani, yataambatana na sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
MATOKEO yalivyotangazwa kwenye tovuti maalumu ya kampeni ya Nani Mtani Jembe, yanaonesha kuwa timu ya Yanga inaongoza kwa kuwa na Sh 55,600,000 huku Simba ikiwa na Sh 44,400,000, ikiwa ni baada ya Simba kuongoza kwa takribani wiki mbili sasa.
UONGOZI wa Klabu ya Simba, leo unakutana na matawi yote ya wanachama ya klabu hiyo ya Dar es Salaam katika mkutano ambao pamoja na mambo mengine, utafanya tathmini ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya soka ya Tanzania uliomalizika Novemba 7, mwaka huu.
ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa timu ya Azam FC, Stewart Hall amepata ulaji mpya baada ya jana kujiunga na Klabu ya Sunderland AFC ya Uingereza akiwa Meneja wa ‘Kidongo Chekundu Sports Park’ pamoja na Kituo cha Michezo cha Elite Sports Academy vinavyojengwa Dar es Salaam.
Mchezaji wa Real Madrid, Pepe amesema maoni aliyotoa Sepp Blatter kuhusu Cristiano Ronaldo hivi karibuni yameonesha wazi kuwa FIFA ina upendeleo.
KARIM Benzema amevilaumu vyombo vya habari kwa kuongoza 'mashambulizi' dhidi yake wakati anahangaika kuitafutia mabao Ufaransa. Benzema, 26, aliifungia nchi yake katika ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Australia na kufuatiwa na mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Finland.