UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), unatarajiwa kufanyika Desemba 10, mwaka huu jijini Mbeya. Kwa mujibu wa taarifa ya Rais wa TBF, Mussa Mziya, mwaka huu wa 2013 ndio ambao uongozi wa shirikisho unafikia ukomo wake, na kikatiba inabidi ufanyike uchaguzi kuwapata viongozi wapya watakaoendesha shughuli za shirikisho kwa miaka minne ijayo.