WAANDAAJI wa Tamasha la Krismasi wametangaza kuwa tamasha hilo ambalo litafanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Desemba 25, mwaka huu, pia litafanyika mikoa ya Tanga na Arusha.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond’ leo anatarajiwa kutoa burudani kwa mashabiki wake wa Jiji la Arusha, onesho lililopangwa kufanyika katika viwanja vya Hoteli ya Mount Meru.
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili nchini Kenya, Anastazia Mukabwa, aliyethibitisha kuwa miongoni mwa watakaotumbuiza katika Tamasha la Krismasi litakalorindima kuanzia Desemba 25, mwaka huu, ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki.
UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Ndondi Tanzania (BFT), unafanyika leo mjini Bagamoyo, imefahamika.
KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura amesema mechi kati ya timu ya Vijana ya wanawake ya Tanzania ‘Tanzanite’ dhidi ya Afrika Kusini, itakuwa ngumu kwa sababu tayari wageni hao watakuwa wameisoma mbinu walizotumia kuitoa Msumbiji.
KOCHA Mkuu wa mpya wa timu ya Azam FC, Joseph Omog anatarajiwa kutua leo kwa ajili ya kufanya mazungumzo na klabu hiyo yenye makazi yake Chamazi, Mbagala, jijini Dar es Salaam.
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limewataka wanachama wao ambao ni mikoa na klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, kuingiza kipengele cha Kamati ya Maadili kwenye Katiba zao, na kwamba hazitafanya uchaguzi wowote kabla ya kuhakikisha zinatekeleza agizo hilo.
MABINGWA watetezi wa Kombe la Chalenji, Uganda jana walianza vyema utetezi wa taji lao baada ya kuizamisha Rwanda kwa bao 1-0 katika mechi yao ya ufunguzi kwenye Uwanja wa Nyayo mjini Nairobi, Kenya.
TIMU ya soka ya Viko Pharm inayoshiriki Ligi Daraja la Pili Taifa juzi ilitoka kidedea baada ya kuifunga DESI bao 1-0 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung mjini Zanzibar.
FAINALI ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa timu za Wizara na Taasisi zake zinatarajiwa kuchezwa kesho kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung mjini Unguja.