BONDIA Mtanzania Omari Kimweri “Lion Boy” anayefanya kazi zake Australia, anatarajia kupanda ulingoni Novemba 30, mwaka huu kupigana na Xiong Zhao Zhong kugombea ubingwa wa dunia nchini China.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
MSANII Upendo Nkone amekuwa wa kwanza kuthibitisha kushiriki Tamasha la Krismasi litakalofanyika Desemba 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Joseph Lazaro amesema baada ya kupoteza mchezo wao wa mwisho wa kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu, atakipangua kikosi chake upya kwa kusajili wengine kwa ajili ya kufanya vizuri wakati ujao.
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Zanzibar “Zanzibar Heroes” inayojiandaa na mashindano ya Chalenji, Salum Bausi amesema kukosekana kwa Nassor Said ‘Cholo’ ni pigo kubwa kwake.
KOCHA wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp anaamini Arsenal inaweza kutwaa taji la ligi ya Mabingwa kama itafanikiwa kuikwepa Bayern Munich. Aaron Ramsey aliifungia Arsenal na kuifanya iibuke na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dortmund juzi na kukaa kileleni ikiwa na mechi mbili kibindoni.
UGONJWA wa kidole tumbo umeondoa maisha ya Dj maarufu nchini Rankim Ramadhani aliyefariki jijini Dar es Salaam jana.
CHAMA cha Darts Kinondoni kinatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu wa viongozi Jumapili ya wiki hii.
TIMU nne za soka kutoka Wilaya ya Mvomero, Kilosa, Kilombero na ya Manispaa ya Morogoro zinaumana vikali katika kinyang’anyiro cha kuwania kupanda ligi daraja la tatu ngazi ya Mkoa.
WACHEZAJI wa timu ya soka ya vijana ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20, Tanzanite waliondoka jana kwenda Msumbiji huku wakiomba watanzania kujitokeza kuifadhili timu hiyo.
SIMBA jana ilirudisha matumaini kwenye Ligi Kuu baada ya kuiadhibu Ashanti United mabao 4-2 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.