TIMU ya soka ya Taifa ya Zanzibar, ‘Zanzibar Heroes’ jana ilianza vema michuano ya Kombe la Chalenji baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Sudan Kusini.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
TIMU ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ imeondoka nchini jana kwenda Nairobi Kenya katika michuano ya Chalenji inayoanza leo nchini humo.
KIUNGO wa timu ya soka ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars,’ Frank Domayo amesema ushindani umekuwa ni mkubwa katika kupata nafasi kwenye kikosi cha Taifa, kwani vijana wengi wamekuwa wakijituma na kuwaangusha wakongwe.
KAMPUNI ya Busara Promotions imeandaa onesho maalumu jijini Dar es Salaam kuonesha shoo za baadhi ya wasanii watakaoshiriki Tamasha la 11 la Sauti za Busara.
MWIMBAJI Solly Mahlangu wa Afrika Kusini amekubali kutumbuiza kwenye Tamasha la Krismasi linaloandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya Dar es Salaam.
KAMPUNI ya burudani ya Chief Promoters kwa kushirikiana na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wameandaa mafunzo ya siku moja kwa wasanii wa muziki, watayarishaji na wasambazaji itakayofanyika leo Dar es Salaam.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imezialika mabingwa wa soka wa Vietnam na Jamhuri ya Watu wa China kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Mapinduzi yatakayopamba maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofikia kilele Januari 12, mwakani.
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limezikumbusha klabu zote kuheshimu kanuni na kuzingatia muda wa usajili wa dirisha dogo la usajili ambalo linafungwa Desemba 15, mwaka huu, huku kukiwa hakuna klabu yoyoye hadi sasa iliyosajili mchezaji wa kigeni.
KOMBE la soka la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, linaanza leo nchini Kenya kwa wenyeji Kenya kuwakabili Ethiopia, ikitanguliwa na mechi ya Zanzibar dhidi ya Sudan Kusini.
MKURUGENZI wa Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo amehimiza wapenzi wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupiga picha na Kombe la Dunia la Fifa linalotarajiwa kutua nchini Ijumaa.