NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi amekiri kwamba anasikia uchungu kufuatia kuandamwa na majeruhi. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alicheza dakika 19 katika mechi ambayo timu yake ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Real Betis Novemba 4, ambapo aliumia paja na hivyo kuwa nje ya uwanja kwa wiki sita mpaka nane.
zaidi ya miaka 7 iliyopita
URENO iko mbele kwa bao 1-0 baada ya mechi ya kwanza hatua ya mtoano, lakini leo ikiwa ni mechi ya marudiano kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Sweden kwenye 'Zlatan Arena' kazi bado inaendelea.
RUFAA ya kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 12 jela iliyofunguliwa na mume wa msanii wa filamu nchini, Kajala Masanja, imeahirishwa hadi Novemba 15, mwaka huu.
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa Zanzibar ‘Zanzibar Heroes,’ Salum Nassor Bausi ametangaza majina ya wachezaji 21 watakaoshiriki michuano ya Chalenji nchini Kenya, huku kipa wa Azam FC, Mwadini Ali akiachwa kwa madai kuwa ni majeruhi.
KOCHA Mkuu wa Rhino Rangers ya Tabora, Sebastian Nkoma ameeleza mpango wake wa kuanza kusaka wachezaji wenye uwezo kwenye vikosi mbalimbali vya jeshi nchini ili kuwaongeza kwenye kikosi chake.
ASHANTI United ya Ilala imeilaza Ruvu Shooting ya Pwani kwa bao 1-0 katika michuano ya vijana ya Kombe la Uhai inayoendelea kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani, Boniface Mkwasa amesema leo atakabidhi ripoti kwa uongozi wa timu hiyo baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
DENISE Bannister kutoka Arusha akiwa na boti yao iliyopewa jina la ‘Lal Louve,’ amekuwa mvuvi bora wa mashindano ya Wazi ya Uvuvi ya Tanga Cement 2013 yalimalizika jijini Tanga juzi jioni akijizolea alama 159.
KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Joseph Kimwaga amesema anaamini kuwa nafasi aliyopata kucheza kwenye timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ imetokana na juhudi zake.
WASANII nyota nchini akiwamo mkongwe Joseph Haule ‘Profesa Jay’, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ni miongoni mwa watakaopanda jukwaa moja na wakali wa muziki kutoka Nigeria, Kundi la P Square wiki hii.