KESHO timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars itaikabili Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mechi ya kwanza ya raundi ya awali ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars,’ Mart Nooij ametaja kikosi cha wachezaji 22 watakaochuana katika mechi ya raundi ya mchujo dhidi ya Zimbabwe kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2015, huku kukiwa hakuna hata mchezaji mmoja wa maboresho.
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul ‘Diamond Platnum’ amewataka Watanzania kutambua kuwa tuzo anazoshindania za MTV pamoja na BET ni tuzo za Watanzania wote kwa ujumla.
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Snura Mushi “Mamaa Majanga,” anatarajiwa kupamba mashindano ya Miss Uni-College Temeke 2014 yaliyopangwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Dar Live Mbagala leo.
MABINGWA wa soka wa Mkoa wa Shinyanga, Bulyanhulu FC wameanza kuonesha maajabu baada ya kupata ushindi wa pili kwa kuifunga Navy FC ya Dar es Salaam mabao 3-2 na kufikisha pointi saba kileleni mwa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kituo cha Morogoro, ikifungana na Mji Mkuu (CDA) ya Dodoma.
TIMU ya Ndanda FC ya Mtwara imesema inatarajia kufanya usajili wa wachezaji wanane kwa ajili ya kukiimarisha kikosi hicho kwa maandalizi ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.
NYOTA wa Barcelona, Lionel Messi amekubali mkataba mpya ambao inaaminika utamfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani, klabu hiyo ya Camp Nou imethibitisha.
BARCELONA na Atletico Madrid zinakutana leo katika mechi ya mwisho ya La Liga kwenye Uwanja wa Camp Nou ambayo itaamua bingwa wa Hispania msimu huu. Wageni wataingia uwanjani wakiwa wanaongoza kileleni mwa La Liga kwa pointi tatu dhidi ya wenyeji wao ambao pia ni mabingwa watetezi.
SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) limesema linasaka wadhamini kwa ajili ya kuwaunga mkono kwenye mashindano ya Muungano yatakayofanyika Juni 21, mwaka huu Dar es Salaam.
CHAMA cha Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) kimesema kinatarajia kufanya mafunzo kwa Makocha, Mabondia wastaafu na Majaji kuhusu sheria za mchezo huo na usalama kwa ajili ya kuwawezesha kutumia vizuri kwenye mashindano mbalimbali.