WASANII wanaowania tuzo za MTV Mama kutoka Tanzania, Kenya na Afrika Kusini juzi walifanya onesho la nguvu katika klabu ya Bilicanas, ikiwa ni moja ya kampeni kuelekea utoaji wa tuzo hizo.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
WABUNGE wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, wameitaka serikali kupiga marufuku vitendo vya kudhalilisha wanawake vinavyoendelea, ikiwemo ngoma za kangamoko na kigodoro kantangaze ambazo zimekuwa zikishamiri katika siku za hivi karibuni.
KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ leo kitakuwa na kibarua wakati itakapopambana na timu ya taifa ya Zimbabwe, ukiwa ni mchezo wa raundi ya kwanza wa kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika zilizopangwa kufanyika Morocco mwakani.
MWIGIZAJI na Mwongozaji wa Filamu Tanzania , Adam Philip Kuambiana amefariki dunia jana saa nne asubuhi wakati akikimbizwa katika Hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
WAZEE wa Baraza la Yanga kwa kushirikiana na jopo la ujenzi wa Uwanja wa Kaunda umesema kesho utatinga kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na barua ya kumkumbusha ahadi yake ya kutekeleza ombi lao juu ya nyongeza ya eneo la ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira.
TIMU ya taifa, Taifa Stars jana iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Zimbabwe katika mchezo wake wa kwanza wa mchujo kuwania kufuzu kwenye makundi ya fainali za mataifa ya Afrika mwakani, mashindano yanayotarajia kufanyika nchini Morocco.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amesema Tanzania inaweza kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika mwakani kutokana na mipangilio mizuri iliyopo chini ya rais mpya wa Shirikisho la soka nchini TFF, Jamali Malinzi.
WACHEZAJI 22 wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, kuogelea na riadha wanaondoka nchini leo kuelekea jijini Gaborone nchini Botswana kushiriki mashindano ya Vijana ya Olimpiki yaliyopangwa kuanza Mei 22 hadi 31 mwaka huu.
TIMU ya JKT Ruvu Jumatatu Mei 19 itaanza mchakato wa kutafuta wachezaji wapya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye uwanja wa JKT Mlalakuwa jijini.
WASANII nchini wameendelea kupaza kilio chao kwa serikali dhidi dhuluma inayotokana na wizi wa kazi zao licha ya juhudi zinazofanywa na mamlaka mbalimbali dhidi ya maharamia hao.