MSHAMBULIAJI wa England, Wayne Rooney ana imani atapewa unahodha wa Manchester United, lakini amesisitiza kwamba hana tatizo kama Robin van Persie atapewa nafasi hiyo.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
CHELSEA ipo kwenye mazungumzo ya awali na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain juu ya kumuuza beki David Luiz kwa ada ya karibu pauni milioni 40.
WADHAMINI zaidi wa hapa nchini wamejitokeza kudhamini shughuli mbalimbali za Tamasha la Filamu la Kimataifa la Zanzibar ZIFF. Miongoni mwa kampuni hizo ni pamoja na Kampuni ya Comnet Zanzibar ambayo imejitolea kudhamini mashindano ya ngalawa.
CHAMA cha Netiboli Tanzania (CHANETA) kimewataka wachezaji wote watakaochaguliwa kwenye timu ya Taifa kuwa na hati ya kusafiria ili kunapotokea safari za kimichezo za nje kuwe rahisi kupeleka taarifa zao.
FAINALI ya michuano ya soka ya ufukweni (beach soccer) kati ya timu za Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) inachezwa leo kwenye ufukwe wa Escape One uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.
MWANAMUZIKI Amina Ngaluma ‘Japanese’ aliyefariki dunia wiki iliyopita nchini Thailand amezikwa jana kwenye makaburi ya Machimbo Mnarani Dar es Salaam.
TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki na Malawi (Flames) keshokutwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwenye vyombo vya habari jana, mechi hiyo itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni.
VIBWEKA vya hapa na pale vilitawala Gymkhana Dar es Salaam jana, wakati kamati ya uchaguzi ya Simba chini ya Mwenyekiti wake Damas Ndumbaro, iliposikiliza mapingamizi waliyowekewa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio katika mechi ya kimataifa ya kirafiki kati ya timu ya Taifa, Taifa Stars na Malawi, itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kesho.
TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, ‘Ngorongoro ‘Heroes’ juzi iliaga michuano ya Afrika baada ya kufungwa mabao 4-1 na wenzao wa Nigeria.