TIMU za Tanzania zitakazoshiriki Michezo ya Jumuiya ya Madola baadaye mwezi huu jijini Glasgow, Scotland, zimeanza kurejea nchini kutoka kambi za mazoezi nje ya nchi, huku zikitamba zimeiva kwa michezo hiyo. Michezo ya Jumuiya ya Madola imepangwa kuanza Glasgow kuanzia Julai 23 hadi Agosti 3, mwaka huu.