TIMU ya Ndanda FC ya Mtwara ambayo kwa mara ya kwanza inaingia kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, inatarajia kuweka kambi yake Dar es Salaam.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
MASHINDANO ya Michezo ya Shirikisho la Michezo ya Shule za Sekondari ya Afrika Mashariki (FEASSSA), yatafanyika jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia Agosti 22 hadi 30, imeelezwa.
MWIMBAJI mahiri nchini, Rose Muhando anatarajia kutambulisha kwa mashabiki wake albamu ya Kamata Pindo la Yesu Agosti 10, mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
MDAU wa michezo mkoani Pwani, Kanali mstaafu Iddi Kipingu amesema atahakikisha mkoa huo unanyakua ubingwa wa mashindano ya riadha ya Taifa ya mwaka huu, baada ya mwaka jana kushika nafasi ya pili nyuma ya Zanzibar ambao walikuwa mabingwa wa jumla ya michuano hiyo.
RAIS mpya wa Klabu ya Simba, Evans Aveva amesema moja ya kazi zake ni kuhakikisha anaiandaa timu hiyo katika ubora wa hali ya juu ili ifanye vizuri na kurudisha watu wao ambao wamehamia Azam FC.
MWIMBAJI maarufu wa nyimbo za Injili, John Lisu atamsindikiza mwimbaji Rose Muhando katika uzinduzi wa albamu ya mwimbaji huyo wa kike, ya Kamata Pindo la Yesu, Agosti 3, mwaka huu.
WAIMBAJI mahiri wa muziki wa Injili wanatarajiwa kuimba wimbo maalumu wa kuhamasisha amani na upendo nchini, wakati wa uzinduzi wa albamu ya Rose Muhando, Kamata Pindo la Yesu Agosti 3, mwaka huu.
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa msaada wa vifaa vya michezo wenye thamani ya Sh milioni 1.1 kwa timu ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF).
MBUNGE wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla amegawa vifaa vya michezo kwa timu za soka za kata 23 zilizopo wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kuanza rasmi kwa kinyang’anyiro cha Kombe la Makalla linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai 15, mwaka huu.
WAZIRI Mkuu wa zamani na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ameutaka uongozi mpya wa Klabu ya Simba kutolipiza kisasi au kufukua maovu ya uongozi uliopita na badala yake kujikita katika kuweka mikakati ya kuendeleza klabu.