TIMU ya soka ya Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar (ZASWA FC) wameendeleza wimbi lao la ushindi kwenye ziara ya siku nne kisiwani Pemba kufuatia ushindi wa bao 1-0 waliopata dhidi ya kikosi mchanganyiko cha Mabingwa wa ligi daraja la pili na la tatu cha Wilaya ya mkoani.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
TIMU ya watoto ya mchezo wa mpira wa kikapu imerejea jana kutoka Canada ilipokwenda kushiriki mechi ya kirafiki ya watoto ya mchezo huo iliyoshirikisha nchi mbalimbali kutoka Ulaya.
TIMU ya kuvuta kamba ya wanaume ya Wizara ya Uchukuzi, imefanikiwa kuwaangusha wababe wa Idara ya Uhamiaji kwa mivuto 2-0 katika mchezo mkali uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri wa mjini hapa.
CASTLE Lager kupitia ushirikiano wake na FC Barcelona, leo inaanza kusajili timu zitakazoshiriki shindano la Castle Lager Perfect 6 la mpira wa miguu litakalohusisha wachezaji sita kila upande linalofanyika kitaifa.
WADAU wa muziki nchini wameaswa kuendelea kuwapigia kura wasanii wanaotaka washinde kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo za muziki za Kilimanjaro zinazotarajiwa kufanyika Mei 3, Dar es Salaam.
NAHODHA msaidizi wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Paul Bundala amewataka watanzania kuwaunga mkono.
KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Van Der Pluijm amesema atawaacha wachezaji wakongwe pamoja na wale waliokosa namba chini yake, kwani lengo ni kutumia wachezaji wenye umri mdogo zaidi msimu ujao.
BENKI ya Exim imejikita katika kusaidia maendeleo ya michezo nchini hususan riadha, ambao kwa siku za nyuma umekuwa ukipeperusha bendera ya Tanzania dhidi ya mataifa mengine katika mashindano ya kimataifa.
TIMU ya Taifa ya Kuogelea imeahidi kufanya vizuri katika mashindano ya kuogelea ya Afrika (CANA) kanda ya tatu na nne yanayotarajiwa kuanza leo Kampala, Uganda.
ZAIDI ya wachezaji wa soka chipukizi 72 kutoka nchi 12 barani Afrika, jana walianza kliniki ya siku tano ya kimataifa ya soka itakayoendeshwa na makocha kutoka Klabu ya Manchester United.