loader
Dstv Habarileo  Mobile

Nyumbani Michezo

Mpya Zaidi

Mtibwa Sugar haitaki mbwembwe kusajili

Mecky MaximeKOCHA Mkuuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime amesema wachezaji wengi waliopo katika kikosi chake ni wazuri hivyo, hategemei kufanya usajili mkubwa kwa ajili ya kujiimarisha msimu ujao.

Akizungumza na gazeti hili, Maxime alisema ndani ya Mtibwa kuna wachezaji wengi wazuri hivyo, hakuna mchezaji aliyempendekeza kwa ajili ya kuachwa isipokuwa kuna nafasi chache zitaongezwa kwa usaidizi.

“Hakuna mchezaji niliyempendekeza kumuacha, kwasababu niliona wapo wengi wazuri, ila kuna nafasi chache tu za usaidizi zitaongezwa baadaye, naamini waliopo wote ni wazuri,” alisema Maxime.

Alisema hata kama usajili utafanyika, wanasubiri kwanza fujo zimalizike kwa baadhi ya timu kubwa ndipo wafanye maamuzi yao. Alisema anatarajia kukabidhi ripoti yake kwa uongozi wa klabu hiyo kabla ya kumalizika kwa wiki hii.

Awali, katika mazungumzo na Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alisema licha ya wachezaji wake kujitahidi, wana mategemeo ya kufanya usajili kutegemeana na mapendekezo ya kocha wao.

Alisema pia anatarajia kufanya mazungumzo na kiongozi wake na kuona kama inafaa kufanya usajili wa wachezaji wachache ili kutengeneza kikosi ambacho kitasaidia kufanya vyema msimu ujao.

“Bado sijakutana na kiongozi wangu, nina mgonjwa, tutawaeleza kama tutafanya usajili kwani tunasubiri kupeleka ripoti ya kocha kwa kiongozi wetu aliyeko Dar es Salaam na kujadili ni kwa vipi tuboreshe kikosi chetu kwa msimu ujao,” alisema Kifaru.

zaidi ya miaka 6 iliyopita