MASHINDANO ya Klabu Bingwa Wavu Mkoa wa Dar es Salaam, yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Jumatano ijayo na kushirikisha zaidi ya timu 15 za wanaume na wanawake.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
MASHINDANO ya shule za sekondari kusaka timu bora zitakazoshiriki michuano ya Sekondari Afrika Mashariki yanatarajiwa kuanza leo kwenye Uwanja wa Lugalo, Dar es Salaam.
MSHINDI wa Kombe la Hepautwa ambayo ni ligi mpya ya mpira wa soka mjini Iringa, atazawadiwa Sh milioni moja taslimu pamoja na kombe.
TIMU ya soka ya Jimbo la Amaan imeitambia Kwamtipura kwa kuifunga mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Majimbo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Mao Tse Tung mjini Unguja.
TAMASHA la Simba jana liligeuka huzuni kwa mashabiki wa klabu hiyo baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-0, katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zesco United ya Zambia uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
MABINGWA watetezi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), Vital’O ya Burundi imeanza kwa kishindo baada ya kuibamiza Banadir ya Somalia kwa mabao 5-1.
KAMATI ya Ufundi ya Riadha Tanzania (RT), imetakiwa kuvunjwa baada ya wanariadha wa Tanzania kuchemsha katika Michezo ya 20 ya Jumuiya ya Madola licha ya kutegemewa kufanya vizuri.
MAOFISA wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), wanawasili leo kuangalia jinsi mchezo huo unavyoendeshwa nchini. Kulingana na taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana kwa vyombo vya habari, ujumbe huo ni wa maofisa sita.
ARSENAL imeonesha dhamira yake ya kufanya vyema msimu huu baada ya kuibamiza Manchester City mabao 3-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii leo kwenye Uwanja wa Wembley jijini hapa.
AZAM FC jana ilipata ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya KMKM katika Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mjini Kigali.