AZAM FC jana ilijiweka pazuri katika kucheza robo fainali ya Kombe la Kagame baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na timu ya Atlabara ya Sudan Kusini.
zaidi ya miaka 6 iliyopita
TIMU ya wavulana ya Morogoro jana ilifanya mauaji ya maangamizi baada ya kuifunga Mbeya mabao 6-1 katika fainali za taifa za mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
KAMATI ya Mashindano ya Kombe la Majimbo imeyaondoa majimbo matano baada ya kushindwa kukamilisha taratibu za mashindano hayo.
MFUNGAJI anayeshikilia rekodi nchini Ujerumani, Miroslav Klose ametangaza kustaafu soka ya kimataifa. Mshambuliaji huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 36, amefunga mabao 71 katika mechi 137 katika zaidi ya miaka 13 aliyoichezea timu ya Taifa.
KOCHA Mkuu wa Mexico, Miguel Herrera amemshauri Javier Hernandez kuihama Manchester United ili kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.
TIMU ya vijana ya soka ya Que Bac ya Mbagala Kipati, Dar es Salaam imeibuka bingwa wa michuano ya Kombe la Mbagala kwa kuilaza Kipati mabao 2-0.
KLABU ya Yanga imesogeza mbele kwa siku moja safari yake ya Pemba kutokana na msiba wa dereva wao, Maulid Kiula uliotokea usiku wa kuamkia jana.
TIMU ya soka ya Jimbo la Kitope imeendelea kupokea kichapo katika mashindano ya Kombe la Majimbo baada ya juzi kufungwa mabao 2-1 na Jimbo la Dole.
WAJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba, wamependekeza suala la haki za wasanii liwepo katika Rasimu ya Katiba Mpya.
KOCHA mpya wa Simba, Patrick Phiri ametua jana Dar es Salaam na kuahidi kurudisha heshima ya Simba.