Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga na Balozi wa China nchini, Wang Ke wakiweka maua kwenye kaburi la mmoja wa wataalamu wa Kichina waliokufa wakati wa ujenzi wa reli ya Tazara, wakati wa maadhimisho ya utamaduni wa Wachina na usafi wa makaburi yaliyofanyika katika eneo la Gongolamboto, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam jana.