Katibu wa Bunge,Stephen Kigaigai (kulia) akizungumza na Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Dk. Jim Yonazi ofisini kwake mjini Dodoma jana. Kushoto ni Naibu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah. (Picha na Bunge).
zaidi ya miaka 4 iliyopita
Tingatinga la Manispaa ya Dodoma likichonga moja ya barabara zinazozunguka kituo cha mabasi yaendayo mikoani katika viwanja vya Maonesho ya Kilimo Nane Nane, Nzuguni nje kidogo ya Mji wa Dodoma.
Rais John Magufuli akikata utepe kuzindua magari 181 ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwenye hafla iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Watumiaji wa magari hasa daladala katika barabara iendayo kwenye Kituo cha Daladala cha Toangoma wilayani Kigamboni, Dar es Salaam wapo katika wakati mgumu kutokana na hali mbaya ya barabara hiyo inayochangiwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Wasafiri wa basi la kampuni ya Prince Ramigo na wananchi wengine wa Kata ya Nyahua wilayani Uyui wakivuka kwa tahadhari kwenye maji yanayopita kwa kasi yaliyokatisha mawasiliano ya barabara kati ya Itigi na Tabora, kufuatia mvua zilizonyesha
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya Tanzania Standard Newspapers Limited (TSN), Dk Jim Yonazi akichangia mada katika mkutano unaoendelea wa Wanataaluma wa Afrika Mashariki katika Jukwaa la Ushirikiano wa Umma na Sekta Binafsi mjini Nairobi, Kenya.
Rais John Magufuli akiagana na Waziri wa Ulinzi wa Israel, Avigdor Lieberman baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Ikulu, Dar es Salaam jana.
Mwandishi wa habari wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) aliyekuwa katika kitengo cha Daily News Digital, Katuma Masamba (24) amefariki dunia. Kifo hicho kilitokea jana jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke mkoani Dar es .
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akionesha zawadi aliyokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Rais John Magufuli akimshukuru Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Laay baada ya Benki hiyo kuchangia mfuko wa elimu wa mkoa wa Geita, kwa kutoa Shilingi milioni 50 kabla ya ufunguzi wa Tawi la benki hiyo mjini Chato jana.