Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mkoani Mtwara yenye urefu wa kilomita tatu, akiwa ziarani mkoani humo jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
mwaka 1 uliopita
Rais wa Rwanda, Paul Kagame akizungumza na wajumbe wa mkutano wa 15 wa kila mwaka wa viongozi wa Serikali nchini humo unaofanyika katika Chuo cha Mafunzo Cha Jeshi la Ulinzi Rwanda, Gabiro. Zaidi ya maofisa 300 wa Serikali kuu na Serikali za mitaa wanahudhuria mkutano huo wa siku nne. (Picha na mtandao).
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akiangalia alama ya mpaka baina ya Tanzania na Kenya eneo la Serengeti wilayani ya Tarime, mkoa wa Mara wakati wa ziara yake ya kukagua mpaka wa nchi hizo aliyoifanya wilayani humo mwishoni mwa wiki. Wengine ni Maofisa wa Serikali na taasisi zake. (Na Mpigapicha Wetu).
Rais John Magufuli akiagana na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Medard Kalemani baada ya kuhudhuria Ibada ya misa takatifu katika Kanisa la kigango cha Mlimani (Parokia teule ya mlimani) wilayani Chato, mkoa wa Geita jana. (Picha na Ikulu).
Rais John Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta walipokutana juzi katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika nchini Uganda. Wa pili kushoto ni Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir.
Rais John Magufuli akisalimiana na mabalozi mbalimbali Ikulu, Dar es Salaam juzi kabla ya kuanza kwa hafl a ya kukaribisha mwaka mpya kwa Mabalozi hao.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwajulia hali mabinti pacha walioungana, Consolata na Maria Mwakikuti ambao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dar es Salaam jana.
"Serikali imebatilisha milki za mashamba yasiyoendelezwa Wilayani Monduli Mkoani Arusha na kuyarudisha kwenye Halmashauri" - Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula. Dodoma.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma, (UDOM) wakifuatilia kikao cha Bunge kikiendelea Bungeni Mkoani Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk Adelardus Kilangi akila kiapo cha uaminifu Bungeni Mjini Dodoma asubuhi hii.